Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli anawatangazia kuwaita kwenye usaili wa maandishi waombaji wa kazi waliofuzu vigezo vya nafasi ya kazi ya AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III iliyotangazwa 11.02.2020.
Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
Usaili ni wa maandishi, utaanza saa 3.00 kamili asubuhi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Monduli tarehe 18/03/2020.
Unatakiwa kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha mkazi, kupiga kura, kazi, hati ya kusafiria.
Unatakiwa kuja na vyeti halisi (Orginal Certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita na astashahada kutegemeana na sifa za mwombaji
“Testimonials”, “Provisional Results”, “statement of results” hati za matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI SLIPS) HAVITAKUBALIKA.
Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo endapo barua zao za maombi zilitufikia, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa.
Nawatakia kila la heri:
Ulaya; S.A.
Mkurugenzi Mtendaji (W),
MONDULI.
kuona majina bofya hapa Orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili Monduli DC.pdf
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli