• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Monduli District Council
Monduli District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Malengo
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Eneo la Utawala
      • Tarafa
      • Kata
      • Vijiji
    • Idara
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Idara ya Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwezekaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Onana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelezwa
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria ndogo
    • Mipango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MACHINJIO YA KISASA YAZINDULIWA MONDULI

Posted on: January 3rd, 2019

Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Idd Hassan Kimanta pamoja na mbunge wa jimbo la Monduli Mhe. Julius Kalanga wamezindua machinjio ya kisasa katika kata ya Makuyuni wilayani Monduli. Uzinduzi huu ulifanyika mwishoni mwa mwezi  desemba 2018. Machinjio haya yako eneo la shamba la manyara Ranch.

 Ni nini hasa wasifu wa Manyara Ranch?

Ranchi ya manyara ina eneo lenye ukubwa wa hekta 17,800 na liko kwenye ushoroba wa wanyama pori unaounganisha Hifadhi za Taifa za Tarangire na Ziwa Manyara. Mwaka 2000, Ranchi ya Manyara ilibinafsishwa kutoka kwenye usimamizi wa Kampuni  za Ranchi za Taifa (NARCO) na kukabidhiwa kwa Tanzania Land Conservation Trust (TLCT), ikiwezeshwa na AWF. TLCT ni chombo kilichoundwa kwa ajili ya kusimamia na kuendesha shughuli zote ndani ya Manyara Ranch. TLCT inajumuisha Vijiji vya Oltukai na Esilalei ambavyo ndivyo vyenye dhamana ya kusimamia na kuendesha shughuli za ufugaji pamoja na hifadhi ya ushoroba wa wanyama pori. Aidha eneo lililotengwa kwa ajili ya shughuli za Machinjio ni hecta 10 tu.

Ni nani anamiliki  Machinjio hayo  kwa sasa?

Kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ndiyo yenye dhamana na usimamizi wa machinjio hii baada ya Serikali kuhuisha Hati ya umiliki wa Shamba la Manyara Ranch kutoka kwa Tanzania Land conservation Trust (TLCT) kwenda kwa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa manufaa ya Vijiji vya Oltukai na Esilalei.

Je machinjio hiyo imejengwa kwa shilingi ngapi? 

Ujenzi wa jengo la Machinjio ya Makuyuni ulianza mwaka 2009 na hadi sasa haujamalizika. Gharama ya ujenzi wa jengo hili  umeshagharimu jumla ya shilingi za Tanzania Shs.448,914,882/=.kwa mchanganuo ufuatao, ujenzi wa jengo la machinjio ni Tsh. 223,514,882 na ununuzi wa Mashine na vifaa vingine  kwa ajili ya Machinjio viligharimu jumla ya Tshs.225,400,000/=.Ujenzi huu uligharamiwa na mtaji wa fedha (grant) kutoka USAID kupitia shirika la African Wildlife Foundation (AWF).

Kuanzia mwaka 2010 utaratibu uliandaliwa wa kuendesha machinjio hii ya Kisasa ikiwa ni pamoja na juhudi za kufanya mchakato wa kumpata mwekezaji atakayekodisha Machinjio hii, ili aweze kuingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli na kuanza kazi ya uzalishaji. Tangu kipindi hicho (2010 hadi 2017)Tenda ilitangazwa lakini hadi sasa bado hajapatikana mwekezaji ambae ameonesha  dhamira/nia  ya kuwekeza.

Je, halmashuri ina mpango Mpango gani wa baadae, baada ya machinjio kukamilika?

Mpango wa baadae wa Machinjio hii ni Pamoja na kupanua wigo wa vyanzo vya mapato yanayotokana na kuuza mifugo na nyama iliyo bora katika kiwanda hicho, kutoza ushuru wa pango kutoka kwa mwekezaji atakaefanikiwa kuendesha kiwanda hicho. Sambamba na hilo kiwanda kitatoa soko la kuuza mifugo na nyama  katika Vijiji  vinavyozunguuka Machinjio.Pia itatoa ajira kwa wananchi ikiweka  kipaumbele kwa jamii zilizo jirani na machinjio hiyo.

Je, kuna Changamoto zozote zinazosababisha   machinjio yasifanye  kazi kwa ufanisi?.

Zifuatazo ni changamoto/mapungufu yanayosababisha machinjio kutofanya kazi kwa ufanisi wake.

  • Kutomalizika kwa mradi
  • Kukosekana kwa mwekezaji
  • Kukosekana fedha za kumalizia ujenzi
  • Vifaa vilivyotumika katika ujenzi huu vina ubora wa kiwango cha chini
  • Mradi haukuwekewa mipango endelevu.

 

 Ni mikakati gani iliyowekwa ya kukabiliana na changamoto hizo? 

  • Mazungumzo yanaendelea na Taasisi za Serkali na zisizo za Serikali, Wafadhili na mashirika mbalimbali kutafuta fedha kwa ajili ya  kumaliza ujenzi wa jengo, kukarabati sehemu zilizochakaa na ununuzi wa vifaa vilivyo na viwango vinavyokubalika .
  • Juhudi zinafanyika za kumpata mwekezaji wa kuendesha mradi huo, ambapo hadi sasa mwekezaji mmoja toka machinjio ya Dodoma amefika na kufanya tathimini ya kitaalamu na tunasuburi mrejesho.

Asanteni; Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2019.

Matangazo

  • MACHAGUO YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • MAAGIZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 (JOINING INSTRUCTIONS) December 18, 2020
  • KUITWA KWENYE USAILI March 13, 2020
  • WALIOITWA KWENYE USAILI WA MAHOJIANO VEO III June 17, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC KIMANTA ASISITIZA MAMBO 3 AKIWA MONDULI.

    June 26, 2020
  • MKUU WA WILAYA YA MONDULI MHE.ACP EDWARD JOTHAM BALELE APOKELEWA KWA KISHINDO MONDULI.

    June 26, 2020
  • MONDULI YAPAMBANUA JINSI ILIVYOJIPANGA KUKABILIANA NA COVID19

    April 07, 2020
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGIA NA KIDATO CHA KWANZA 2020 MONDULI

    December 09, 2019
  • Angalia zote

Maktaba ya Video

WANAWAKE WANUFAIKA NA MAMILIONI YA FEDHA KUTOKA HALMASHAURI- MONDULI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • EDWARD MORINGE SOKOINE
  • TAARIFA YA UPANDAJI MITI
  • Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
  • Mto Wa Mbu - Monduli ilivyonufaika na Tsh. Milion 400

Viunganishi linganifu

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya ajira ya Serikali
  • Ofisi ya Rais utumishi na utawala bora
  • salary slip portal

Waliotembelea Kiulimwengu

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Monduli District Council

    Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli

    Namba ya simu: +255 - 27- 2538006

    simu ya mkononi:

    Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz

Mawsilano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Malalamiko
    • ramani ya eneo
    • Huduma zetu

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli