IDARA FEDHA NA BIASHARA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI
Maombi yote mapya ya Leseni za Vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye fomu ya maombi, (Afisa Afya, Afisa Ardhi, Afisa Biashara, Polisi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata husika.
LESENI ZA VILEO:
Biashara ya Vileo inatekelezwa kwa kufuata Sheria ya Mwaka 1968, kifungu 28 (Liquor Licence Act No. 28 of 1968) na Marekebisho ya Sheria hiyo yaliyofanywa 2004.
UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA LESENI ZA VILEO:
Maombi yote yanayorudiwa (Renewal) yapitishwe na Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo Kata na yawasilishwe kwa Afisa Biashara anayeshughulikia Leseni za Vileo kwa utekelezaji.
Maombi yote mapya ya Leseni za Vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye fomu ya maombi, (Afisa Afya, Afisa Ardhi, Afisa Biashara, Polisi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata husika
Aidha wanaoendesha biashara ya Vileo bila kufuata taratibu zilizotajwa hapo juu huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani kulipishwa faini pamoja na penalty au kufungiwa biashara zao.
KODI YA MAPATO
Kwa nini watu wanalipa Kodi?
Kodi ndicho chanzo pekee cha uhakika cha Serikali yoyote duniani cha mapato yake, ingawa katika falsafa ya kodi kuna sababu nyingine za kutoa kodi.
Mfano:-
- Kulinda tabia za watu
- Kulinda viwanda
- Kupambana na mfumuko wa bei
- Kushawishi uwekezaji
- Kupunguza kipato kati ya mtu na mtu
- Kuhamisha utajiri wa sehemu moja kwenda nyingine n.k.
Halmashauri wilaya ya Monduli hupata mapato kutokana na vyanzo vikuu ambavyo ni.
(i) Mapato yake yenyewe
(ii) Ruzuku kutoka Serikali Kuu
(iii) Misaada ya wahisani
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli