Mhe. Isack Joseph Copriano Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Monduli leo Feb.5, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo, ameongoza Baraza la Madiwani lenye dhima ya kupokea na kujadili rasimu ya Mpango wa mapendekezo ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Akiongoza majadiliano katika Baraza hilo, Mhe. Isack Copriano, wajumbe pamoja na Wataalamu katika Halmashauri hiyo wamepitisha rasimu ya bajeti yenye jumla ya fedha za Kitanzania bilioni 48.1 ikiwa na ongezeko la asilimia 3.4 ukilinganisha na shilingi bilioni 46.5 za bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo fedha hizo zitakusanywa na kutumiwa katika shughuli mbalimbali za Maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa Mwaka wa fedha 2025/2026.
Sambamba na kupitisha bajeti hiyo, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kwa kufurahishwa na jitihada zilizopelekea ongezeko la mapato ya ndani kwa asilimia 3.4, limeruhusu gari lililokuwa likitumiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuanza kutumiwa na Idara ya fedha na uhasibu ili kuendelea kuboresha na kudhibiti shughuli za ukusanyaji mapato Wilayani humo
Vilevile, Baraza la Madiwani Wilaya ya Monduli limeelekeza shilingi milioni 150 zitengwe kwa ajili ya manunuzi ya gari la Idara ya Maliasili na Mazingira ili kuwezesha Idara hiyo kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi
Mhe. Isack Copriano amehitimisha Baraza hilo kwa kuwataka Wataalamu Wilayani humo kufanya maboresho katika bajeti hiyo sawa sawa na maamuzi ya Baraza hilo huku akisisitiza miradi pendekezwa kwenye bajeti ya 2025/2026 izingatiwe.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli