Naamini sisi kama Viongozi vijana tuna malengo ya kufika mbali endapo tutawajibika kwa nafasi tulizo aminiwa. Hivyo ninaelekeza Wenyeviti wa Vijiji na Wenyeviti wa Vitongoji wote kuweni karibu na Wananchi. Kiongozi yeyote ambaye hawezi kukaa karibu na wananchi akae pembeni atafutwe anayeweza kukaa karibu na wananchi.
Hayo yamesemwa leo Novemba 19, 2025 na Mhe. Gloriana Kimath Mkuu wa Wilaya ya Monduli alipokuwa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mtimmoja Kata ya Sepeko Wilayani Monduli katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji wa a Kata eneo la Mtimmoja.
Katika ziara hiyo Mhe. Gloriana ameeleza lengo la ziara yake Kijijini hapo kuwa ni kujitambulisha kwa Wananchi hao, kusikiliza na kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hao ndani ya kijiji hicho.
Aidha, katika kutatua migogoro ukiwemo mgogoro wa ardhi baina ya Wananchi na Mwananchi aitwaye Ndg. Ndekenya Laizer, Mhe. Gloriana ametangaza rasmi eneo la ardhi linalomilikiwa na Mwananchi huyo kuwa amelirudishwa rasmi kwa wananchi baada ya eneo hilo kuwa na mgogoro wa muda mrefu baina yao na kwamba Mwananchi huyo alilichukuwa bila kufuata taratibu zinazotakiwa.
Aidha Diwani Mteule wa kata ya Sepeko Mhe. Diwani Kimaai Teretui amesema “ikitokea labda kuna mahali Kiongozi ameteleza au Mwananchi ameteleza tuitane tukae chini tutatue”. amesema Mhe. Diwani
Kwa upande wao wakazi wa kata ya Sepeko wakiwakilishwa na Mzee Raphael N. Mollel wamemuomba Mhe. Gloriana Mkuu wa Wilaya ya Monduli kutenga siku maalum ili afike tena kusikiliza kero zote za wananchi na wapate suluhu zinazowakabili hasa upande wa wanyama wakali kama Tembo.
Akizungumzia suala la uharibifu unaofanywa na tembo katika maeneo hayo Ndg. Msuya Natashoo Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Maliasili, amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa Vijana kuhusu matumizi ya vifaa vya kuzuia Wanyama hao na namna ya kukabiliana nao ili wasiingie kwenye makazi ya watu na kuleta uharibifu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli