• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Monduli District Council
Monduli District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Malengo
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Eneo la Utawala
      • Tarafa
      • Kata
      • Vijiji
    • Idara
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Idara ya Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwezekaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Onana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelezwa
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria ndogo
    • Mipango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

DC KISWAGA AZUNGUMZA NA WATUMISHI IDARA YA AFYA MONDULI

Posted on: September 10th, 2024

Mhe. Festo S. Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Monduli Leo Septemba 10, 2024 amefanya kikao na watumishi wa Idara ya Afya wa Hospitali ya Wilaya ya Monduli chenye lengo la kuwakumbusha wajibu na majukumu yao ya kazi ambayo kwayo Serikali imewaamini na kuwaajiri ili wawahudumie Wananchi kiafya Kwa maendeleo ya Taifa letu.

" Nimeona tuzungumze kama familiya Kwa kuwa sisi sote tunafanya kazi za kuwahudumia Wananchi wa Wilaya yetu ili tuwekane sawa na tutoe Huduma nzuri Kwa Wateja wetu. Na kwakuwa ninyi mmeaminiwa na Serikali mnapaswa kutoa Huduma kwa haki na kwa wakati. "  Amesema Mhe. Kiswaga

Akizungumza na watumishi hao wa afya Mhe. Kiswaga amesema kutokana na uwepo wa malalamiko mengi anayoyapokea kutoka kwa Wananchi, imeomekana dhahiri kuwa utendaji kazi wa watumishi hospitalini hapo si mzuri jambo linalopelekea wananchi kulalamika ya kwamba wanapoteza muda mwingi kusubiria kupata huduma jambo linalochelewesha  watu kupona na kuendelea na shughuli za maendeleo.

Mhe. Kiswaga ameongeza kuwa wagonjwa wanakaa muda mrefu bila kupata huduma kwani watoa huduma wanakuwa hawapo Katika maeneo yao ya kazi (ofisini) wakazi wa kazi.Amemtaka Mganga Mkuu huyo kumwandikia taarifa inayo onyesha ni wapi wagonjwa hao wanacheleweshwa kupata huduma mara wanapofika hospitalini hapo.

Sambamba na hayo Mhe. Kiswaga amebaini kuwa wapo watumishi ambao wamekuwepo Katika eneo hilo la kazi (Hospitali ya Wilaya ya Monduli) Kwa miaka zaidi ya 20 jambo ambalo amewataka wasizoelee kazi Wala mazingira bali watumie fursa hiyo na weledi walionao kufanya kazi kwa ufasaha na ufanisi mkubwa.

Aidha, Mhe. Kiswaga amemtaka Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. George Kasibante kuandaa mafunzo ya siku mbili ndani ya wiki mbili zijazo ili watumishi wote wa afya hospitalini hapo wakumbushwe na kufundishwa juu ya suala la huduma Kwa Wateja hatimaye wajitambue na kukumbuka wajibu wao Kwa Wananchi wanao wahudumia, na katika mafunzo hayo ameahidi kuwa Mgeni rasmi atakae yafungua.

Ameongeza kuwa baada ya mafunzo hayo sitegemei tena Mganga Mkuu awakumbushe kila siku wajibu wenu wa kuwahudumia wananchi bali Kila mmoja wenu ajitambue na kujuwa ni nini anapaswa akifanye kwa manufaa ya Wananchi.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. George Kasibante amejibu hoja hiyo Kwa kusema Katika maeneo yote anakopitia Mgonjwa ukianzia mapokezi sehemu pekee anakoweza kutumia muda mrefu ni maabara ambako vipimo vya muda mrefu zaidi ni muda wa saa moja (1).

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Laizer amemshukuru Mkuu wa wilaya Mhe. Kiswaga Kwa kuwakumbusha watumishi wa Idara ya afya Wilayani hapo wajibu wao na ameahidi kuwa mafunzo aliyoagiza yatafanyika Kwa wakati. Pia kamshukuru Mhe. Kiswaga kuwa bega Kwa bega Katika kuhakikisha ujenzi wa majengo ya OPD,ufuaji, Mionzi na jengo la upssuaji yanakamilika Kwa wakati.

Mhe. Kiswaga amewasisitiza watumishi hao wa Idara ya Afya kuwa  "umeajiriwa kama mtumishi na hii si kazi ya familiya Wala si eneo la biashara Dr. Samia Suluhu Hassan ametoa pesa nyingi ili kuhakikisha mazingira ya kazi  yanaboreshwa yaani majengo, vifaa tiba na madawa hivyo si vema mwananchi kucheleweshwa anapohitaji Huduma."

Mhe. Festo Kiswaga amehitimisha kwa kumpa mwezi mmoja Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Monduli kuruhusu majengo ya OPD, Mionzi, upasuaji na ufuaji kuanza kutumika kuanzia  Oktoba 10, 2024.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC KISWAGA ASITISHA UJENZI ENEO LA MWEKEZAJI

    May 19, 2025
  • DC MONDULI AWAPONGEZA MADAKATRI BINGWA WA MAMA SAMIA

    May 17, 2025
  • ELIMU YA LISHE, AFYA NA MAZINGIRA PAMOJA NA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE IENDELEE KUTOLEWA- MONDULI.

    May 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI ROBO YA 3

    May 14, 2025
  • Angalia zote

Maktaba ya Video

UFUNDISHAJI WA SOMO LA HISABATI KWA VITENDO KWA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI MAZOEZI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • EDWARD MORINGE SOKOINE
  • TAARIFA YA UPANDAJI MITI
  • Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
  • Mto Wa Mbu - Monduli ilivyonufaika na Tsh. Milion 400

Viunganishi linganifu

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya ajira ya Serikali
  • Ofisi ya Rais utumishi na utawala bora
  • salary slip portal
  • Tanzania Safari Channel

Waliotembelea Kiulimwengu

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Monduli District Council

    Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli

    Namba ya simu: +255 - 27- 2538006

    simu ya mkononi:

    Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz

Mawsilano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Malalamiko
    • ramani ya eneo
    • Huduma zetu

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli