Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Leo Oktoba 24, 2024 katika Kijiji cha Tukusi Wilayani Monduli Mkoani Arusha, amezindua Mpango wa uchimbaji Visima virefu zaidi ya 30 unaofanyika kwenye Majimbo yote ya Mkoa wa Arusha ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuhakikisha maeneo yote yanakuwa na maji ya uhakika na salama muda wote.
Katika uzinduzi huo, Wizara ya Maji kupitia Bw. Gibson Bayona, ambaye ni Mratibu wa Kampeni ya Maji inayoendelea nchi nzima wenye jina la "Maji Mwa Mwa Mwaa", amba yo utekelezaji wake unatokana na uwezeshaji wa serikali ya awamu ya sita uliotokana na fedha za kupambana na janga la UVIKO-19, ambapo fedha zake zilitumika kununua mitambo 25 ya uchimbaji wa visima virefu na utengenezaji wa mabwawa ya maji kwenye Mikoa zaidi ya 25 ikiwemo Mkoa wa Arusha.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Kiswaga ameeleza furaha yake ya Upatikanaji wa Maji ndani ya vijiji vitano (5) vilivyopo Wilaya ya Monduli ambapo awali vimekuwa na changamoto kubwa ya Maji,huku akitoa shukrani za pekee kwa Mhe Rais wa awamu ya sita kupitia kupitia Wizara ya Maji inayosimiwa na Mhe.Juma Awesome kwa kuwa wana Monduli sasa watapata Maji wastani Lita elfu elfu thelathini (30,000).
Kwa upande wake Mhandisi Naville Msaki ambaye ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Monduli amesema "kupitia programu hii maaalumu ya uchimbaji visima mia tisa (900) Nchini kwa kutumia mtambo wa kuchimba visima Wilaya ya Monduli tumefanikiwa kupata visima vitano katika vijiji vitano (5) ambavyo awali havikuwa na Maji sasa vinaweza kupata Maji kwa mkisio ya Lita elfu thelathini (30,000) kwa saa na vijiji hivyo ni Tukusi,Kilimatinda,Lolera,Oldonyo na Engorika." amesema Mhandisi Msaki
Kwa ujumla,wananchi na wanufaika wa mradi huo wa maji wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwakumbuka, wakimuombea kheri, afya njema na uwajibikaji mwema katika majukumu yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda kwa kuweza kuwafikia.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli