Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Mhe. Gloriana Kimath, amemrejesha rasmi madarakani Mwenyekiti wa Kijiji cha Migombani Kata ya Majengo Wilayani humo Ndg. Festo Philipo ambaye alisimamishwa Majukumu yake ya kazi tarehe 19 Mei 2025 ili kupisha uchunguzi kuhusu mgogoro wa kimkataba kati ya kijiji hicho na mwekezaji Baltazari Michael Msanya ambapo; urejeshwaji wa Mwenyekiti huyo umefanyika leo tarehe 18 Novemba 2025 katika mkutano wa hadhara na wanakijiji wa Kata ya Mingombani.
Akizungumza katika Mkutano huo Mhe. Gloriana amesema kuwa, Uamuzi huo umefikiwa baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa kubaini kuwa Mwenyekiti huyo hana hatia katika mgogoro huo.
Aidha, Mhe. Gloriana Kimath ameagiza mwekezaji huyo (Ndg. Baltazari Michael Msanya) kusitisha shughuli zote za uwekezaji katika eneo hilo hadi mkataba mpya utakapoandaliwa na kusainiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Vilevile, Mhe.Gloriana amewaasa viongozi wa eneo hilo kuwa wawajibikaji kwa kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu, sambamba na kutenda haki katika kutatua migogoro ya wananchi katika maeneo yao.
Naye Ndugu Marshija Hamisi amemshukuru Mhe. Gloriana kwa kumrudisha mwenyekiti wa kijiji hicho kazini kwani ni kwa muda mrefu walikua wakisubiri na hatimae leo anaenda kuanza majukumu yake rasmi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli