• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
Monduli District Council
Monduli District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dhima na Dira
    • Malengo
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Eneo la Utawala
      • Tarafa
      • Kata
      • Vijiji
    • Idara
      • Idara ya Utumishi na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Ardhi na Mali Asili
      • Idara ya Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwezekaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha, Utawala na Mipango
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Elimu, Afya na Maji
      • UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Madiwani
      • Onana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelezwa
  • Machapisho
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria ndogo
    • Mipango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WA MTO WA MBU WILAYA YA MONDULI WALIVYONUFAIKA NA SHILINGI MILIONI 400 ZA MFUKO WA AFYA.

Posted on: May 17th, 2018


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa Tsh. Milioni 400 fedha za ruzuku kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Kituo cha Afya Mto wa Mbu. Kituo cha afya mto wa mbu ni moja ya vituo vya afya nchini vilivyonufaika na fedha za miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Kazi zinazofanyika ni pamoja na ukarabati na ujenzi wa majengo ambayo ni wodi ya wazazi (Maternity ward), Jengo linalojumuisha chumba cha upasuaji (Theater), X-ray, Ultra Sound na maabara, jengo ya kufulia (laundry), nyumba moja ya mtumishi na tanki la maji.

Mradi unasimamiwa na kamati ya Usimamizi, Manunuzi, Ujenzi na Mapokezi. Mradi uko katika hatua ya umaliziaji ambapo kamati ya usimamizi inatarajia kukamilisha na kukabidhi mradi huo kwa Halmashauri mnamo tarehe 30.05.2018 kwa ajili ya kuanza kutumika. Mpaka sasa fedha zilizotumika ni Tsh. 262,735,138/= na kiasi kilichobaki kwa ajili ya kumalizia mradi huu ni Tsh. 137,264,862/=.

Awali Halmashauri ilipeleka kiasi cha Tshs. Milioni 37 na mchango wa Wananchi ulikuwa Tshs. 2,500,000/= ambapo fedha hizo zilitumika katika hatua za awali za ujenzi wa kituo hicho. Mkurugenzi Mtendaji (W) ameshatoa fedha kiasi cha Tsh. Milioni 2 kwa ajili ya kusaidia shughuli za ufuatiliaji na Usimamizi wa mradi huo kutokana na fedha zilizopokelewa kiasi cha Tshs. Mil 400 kutoelekezwa katika usimamizi.

 Kutokana na mradi kutakiwa kutumia nguvu kazi zaidi kutoka kwa Wananchi, kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kutotii wito wa kujitolea nguvu kazi. Aidha wananchi ambao hawakutoa ushirikiano wa nguvu kazi ni pamoja na wanachi wa Kata za Mto wa Mbu, Majengo na Migungani.

Katika ziara ya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ya Halmashauri  iliyofanyika katika eneo la mradi tarehe 12/5/2018, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli walishauri yafuatayo;

  • Viongozi ya Kata ya Mto wa Mbu na Migungani wahamasishe wananchi kujitolea nguvu kazi katika kukamilisha ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya.
  • Katika hatua ya Umaliziaji, Idara ya Ujenzi ihusike zaidi katika kusimamia mafundi ili kazi iwe bora kutokana na muda uliobaki kuwa kidogo. 

Ziara hii ya kamati ya Fedha, Utawala na Mipango ilipitia pia miradi mingine ya maendeleo katika wilaya ya Monduli ambayo ni ujenzi wa bweni la wanafunzi shule ya sekondari Nanja, ujenzi wa madarasa mawili na ukarabati wa bweni katika shule ya sekondari ya Lowassa, ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa Afya katika zahanati ya kijiji cha Arkatani na ujenzi wa mabweni katika shule ya msingi Manyara Ranch. Baadhi ya miradi hii ilikuwa kwenye hatua ya umaliziaji.


 
-------------------------------------MWISHO------------------------------

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI July 04, 2022
  • NAFASI ZA KAZI May 25, 2022
  • NAFASI ZA KAZI ZA ANWANI ZA MAKAZI February 22, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO YA KAZI YA ANUWANI ZA MAKAZI March 24, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • HILI NI LANGO LA UTALII, KUWENI WAKARIMU.

    May 16, 2023
  • KARIBU MONDULI DKT MPANGO

    May 16, 2023
  • KAMATI YA SIASA WILAYA IMEKAGUA MIRADI

    May 02, 2023
  • MAPATO YA NDANI KUJENGA ZAHANATI SELELA

    April 28, 2023
  • Angalia zote

Maktaba ya Video

WANAWAKE WANUFAIKA NA MAMILIONI YA FEDHA KUTOKA HALMASHAURI- MONDULI
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • EDWARD MORINGE SOKOINE
  • TAARIFA YA UPANDAJI MITI
  • Historia ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
  • Mto Wa Mbu - Monduli ilivyonufaika na Tsh. Milion 400

Viunganishi linganifu

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  • Tovuti ya ajira ya Serikali
  • Ofisi ya Rais utumishi na utawala bora
  • salary slip portal
  • Tanzania Safari Channel

Waliotembelea Kiulimwengu

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana nasi

    Monduli District Council

    Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli

    Namba ya simu: +255 - 27- 2538006

    simu ya mkononi:

    Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz

Mawsilano Mengine

   

    • Sera Binafsi
    • Malalamiko
    • ramani ya eneo
    • Huduma zetu

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli